Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:51

Maraisi wa Afrika ya Kusini na Sudan Kusini wakutana Pretoria


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kulia) akizungumza na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa huko Juba, terehe 2 Juni 2015. Picha na REUTERS/Jok Solomun
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kulia) akizungumza na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa huko Juba, terehe 2 Juni 2015. Picha na REUTERS/Jok Solomun

Rais wa Sudan Kusini amefanya mazungumzo na rais wa Afrika Kusini kuhusu mzozo unaoendelea Sudan pamoja na mchakato wenye utata wa kuleta amani Sudan Kusini, Pretoria ilisema Jumatano.

Marais Salva Kiir na Cyril Ramaphosa walitarajiwa kujadili "maswala yenye manufaa kwa pande zote... na mzozo unaoendelea" nchini Sudan, ofisi ya rais wa Afrika Kusini ilisema katika taarifa.

Viongozi hao wawili pia walitarajiwa kutathimini maendeleo ya utekelezaji “wa ufufuaji” wa mkataba wa amani wa Sudan Kusini.

Mgogoro unaoendelea katika nchi jirani ya Sudan, iliyoko kaskazini mwa Sudan Kusini, umewalazimu zaidi ya wakimbizi 100,000 wa Sudan Kusini kuikimbia nchi hiyo na kurejea kwao.

Uhamaji huo umezua hofu ya kutokea mapigano mapya ya kikabila, Umoja wa Mataifa umesema, wakati huo huo watu 13 wakiuawa katika kambi ya ulinzi wa raia mapema mwezi huu.

Baada ya kupata uhuru kutoka kwa Sudan mwaka 2011, Sudan Kusini ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya takriban watu 400,000 na mamilioni kuyahama makazi yao kati ya 2013 na 2018.

Mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2018 ulikuwa na makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Kiir na mpinzani wake Riek Machar katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Lakini kumekuwa na mivutano huku makundi ya wenyeji wenye silaha yakiendelea kutishia nchi hiyo changa zaidi duniani.

Msemaji wa Ramaphosa Vincent Magwenya aliliambia shirika la habari la AFP kuwa ya vyombo vya habari havita ruhusiwa wakati wa mazungumzo ya maraisi hao wawili.

Forum

XS
SM
MD
LG