Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:57

Wabunge wa Marekani wataka A. Kusini isiwe mwenyeji wa Mkutano wa AGOA


FILE - Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakiongea wakati wa Mkutano wa Africa -Russia katika hoteli ya Black Sea, Sochi, Russia, Oct. 23, 2019.
FILE - Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakiongea wakati wa Mkutano wa Africa -Russia katika hoteli ya Black Sea, Sochi, Russia, Oct. 23, 2019.

Hatua hii ya wabunge hao wa Marekani ni katika kujibu kile kinachoelezwa kuwa nchi hiyo kuwa na uhusiano mkubwa wa kijeshi na Russia.

katika barua kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken na maafisa wengine wa juu, wabunge hao pia wamependekeza kwamba Afrika Kusini iko hatarini kupoteza nafuu inayopata chini ya sheria ya biashara huru kati ya Marekani na nchi za Afrika- AGOA.

Afrika Kusini inatarajiwa kuandaa Mkutano wa AGOA huko Johanesburg utakaohusisha viongozi wa Afria na maafisa wa Marekani kujadili mwelekeo wa baadae wa AGOA, mpango ambao muda wake unatarajiwa kumaliza mwaka 2025.

Biashara ya usafirishaji bidhaa za Afrika Kusini kuelekea Marekani imefikia dola za Marekani bilioni moja katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka 2023, na kupelekea taifa hilo kuwa la pili kwa ukubwa kunufaika na Programu hiyo baada ya Nigeria.

Forum

XS
SM
MD
LG