Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema Jumatano kuwa mazungumzo kuhusu kutatua mzozo na Russia hayawezi kuanza kwa kusitisha uhasama pekee.
Kama kuna mtu anadhani anapaswa kuzuia mgogoro huo na kisha kuona namna ya kuutatua, hawajui, alisema katika mkutano kwa njia ya mtandao uliowalenga waandishi wa habari wa Afrika, kufuatia ziara yake ya nchi za Afrika.
Zaidi ya duru 100 za mashauriano na majaribio ya kusitisha mapigano tangu Russia ilipoiteka Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014 ilisababisha uvamizi kamili wa Ukraine hapo Februari 2022.
Ujumbe wa wakuu wa nchi za Afrika unatarajiwa kuzuru Ukraine na Russia katika siku chache zijazo wakiwa na matumaini ya kuwashawishi kusitisha uhasama, msemaji wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema hapo jana lakini amesema hakuna tarehe iliyowekwa kwa ajili ya safari ya ujumbe huo hadi sasa.
Forum