Imepewa jina la kulitambua “Northern/Interaction-2023,” mazoezi hayo yanaadhimisha uimarishaji wa ushirikiano wa kijeshi kati ya China na Russia tangu Moscow ilipoivamia Ukraine na yanafanyika wakati Beijing ikiendelea kukataa wito wa Marekani kurejesha mawasiliano ya kijeshi.
Manowari hiyo ya China inashirikisha meli za kivita tano na helikopta zinazobebwa na manowari hizo nne, ziliondoka bandari ya mashariki ya Qingdao na itaungana na majeshi ya Russia katika “eneo lililopangwa mapema,” wizara hiyo ilisema katika akaunti yake rasmi ya WeChat Jumapili.
Siku ya Jumamosi, wizara hiyo ilisema jeshi la majini na angani litashiriki katika mazoezi yanayofanyika katika Bahari ya Japan.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa majeshi ya Russia kushiriki katika mazoezi hayo, gazeti la serikali Global Times lilieleza yale wasemayo wafuatiliaji wa masuala ya kijeshi.
Gromkiy na Sovershenniy, manowari mbili za Russia zinazoshiriki katika mazoezi ya Bahari ya Japan, mapema mwezi huu zilifanya mafunzo na jeshi la majini la China peke yao huko Shanghai katika kupanga harakati, mawasiliano na uokoaji baharini.
Kabla ya kutia nanga katika kituo cha kifedha cha Shanghai, meli hizo zilikuwa zimesafiri kupitia Taiwan na Japan, zikisababisha Taipei na Tokyo kufuatilia manowari hizo.
Siku kadhaa kabla ya Russia kuivamia Ukraine mwezi Februari 2022, Rais Vladimir Putin na Rais wa China Xi Jinping walitangaza ushirikiano “usiokuwa na ukomo” waliosema unakusudia kudhibiti ushawishi wa Marekani.
Eneo moja maarufu la ushirikiano huo ni ushirikiano wa kijeshi.
Wakati Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu alipokutana na mkuu wa majeshi ya majini wa Russia, Admiral Nikolai Yevmenov, huko Beijing mwezi huu, pande zote zilisisitiza ahadi yao ya kuimarisha mafungamano ya kijeshi.
Mkuu wa wafanyakazi wa Majeshi ya China Liu Zhenli na Mwanajeshi wa Juu wa Russia, Mkuu wa Wafanyakazi Valery Gerasimov ametoa ahadi kama hiyo wakati wa mazungumzo kwa njia ya mtandao wa video mwezi Juni.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.
Forum