Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:08

Russia, China na Iran zakalimisha mazoezi ya kijeshi


Russia, China na Iran zimekamilisha mazoezi ya njia tatu ya jeshi la wanamaji katika bahari ya Arabia ambayo yalijumuisha kulenga shabaha baharini na angani, wizara ya ulinzi ya Russia imesema Jumamosi.

Mazoezi hayo yaliyofanyika nje kidogo ya bandari ya Chabahar nchini Iran, yametekelezwa wakati Rais wa Russia, Vladimir Putin akijiandaa kumkaribisha mwenzake wa China, Xi Jinping mjini Moscow kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu kuanzia Jumatatu.

Russia imeendelea kufanya mazoezi ya kijeshi na washirika wake haswa China, licha ya vikosi vyake vya kijeshi kujikita katika vita vya mwaka mzima dhidi ya Ukraine, ambapo imeshindwa kupata mafanikio makubwa tangu msimu wa joto uliopita.

XS
SM
MD
LG