Wiki iliyopita, Korea Kaskazini ilifanya jaribio la silaha la kichokozi zaidi baada ya miaka mingi, baada ya kurusha kwa mara ya kwanza silaha ya maalum ya bara hadi bara. Silaha hiyo inasemekana kuwa vigumu kugunduliwa na adui na kwamba ina uwezo wa kufika kwenye bara la Marekani.
Jeshi la wanamaji la Korea Kusini limesema Jumatatu kwamba mazoeozi yalifanyikia kwenye maji ya kimataifa karibu na ufukwe wa mashariki mwa taifa hilo, yakilenga mbinu za kugundua na kunasa pamoja na kushirikiana taarifa kuhusu silaha kutoka Korea Kaskazini. Mazoezi hayo ya ziku moja yakihusisha meli ya kivita aina ya Aegis destroyer kutoka mataifa yote matatu.