Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:52

Wanajeshi wa Israel watashiriki mazoezi ya kijeshi nchini Morocco

Mfano wa mwanajeshi wa Israel katika moja ya maeneo ya mazoezi ya kijeshi
Mfano wa mwanajeshi wa Israel katika moja ya maeneo ya mazoezi ya kijeshi

Hii ni mara ya kwanza kwa IDF kushiriki kikamilifu katika mazoezi ya kimataifa ya African Lion ilisema taarifa kutoka jeshi la Israeli Jumatatu jioni. Ujumbe wa wanajeshi 12 na makamanda kutoka kikosi cha Golani Reconnaissance Battalion umetumwa kushiriki pamoja na wanajeshi 8,000 kutoka nchi 18.

Wanajeshi wa Israel kwa mara ya kwanza watashiriki katika mazoezi ya kijeshi nchini Morocco wakati mazowezi makubwa ya kivita barani Afrika yatakapoanza Jumanne, jeshi la Israel limesema.

Hii ni mara ya kwanza kwa IDF kushiriki kikamilifu katika mazoezi ya kimataifa ya African Lion ilisema taarifa kutoka jeshi la Israeli Jumatatu jioni. Ujumbe wa wanajeshi 12 na makamanda kutoka kikosi cha Golani Reconnaissance Battalion umetumwa kushiriki pamoja na wanajeshi 8,000 kutoka nchi 18.

Tukio hilo ambalo sasa lipo katika toleo lake la 19 limeandaliwa na Morocco na Marekani. Katika muda wa wiki mbili zijazo wanajeshi watajizatiti kwenye mafunzo katika changamoto mbalimbali za mapigano ambayo yanajumuisha vita katika maeneo ya mijini na vita vya chini ya ardhi ambapo watahitimisha katika zoezi la kawaida kwa majeshi yote yanayoshiriki, ilisema taarifa ya Israeli.

Forum

XS
SM
MD
LG