Wanadiplomasia wa juu kutoka China, Marekani na Russia ni kati ya wale ambao wanatarajiwa kuhudhuria kikao cha ASEAN Regional Forum (ARF), ambapo ajenda pana zimegubikwa na matukio ya mivutano ya kisiasa ya kieneo ya wiki, ikitoa jukwaa kwa majibizano makali, misuguano ya mataifa yenye nguvu na baadhi ya nchi kususia kikao.
Katika matamshi yake ya ufunguzi kwa mawaziri wa mambo ya nje kutoka Jumuiya ya Mataifa ya Asia Kusini Mashariki (ASEAN), Rais wa Indonesia ambaye ni mwenyekiti Joko Widodo alisema mkusanyiko huo una lengo la kutafuta ufumbuzi kuliko kuendeleza maatizo ya kieneo na kimataifa.
“Sisi, wanachama wa ASEAN ambao bado tunaendelea, tunahitaji uelewano, busara, misaada kutoka nchi zilizoendelea, kutoka nchi majirani zetu, kuweza kuepuka muelekeo wa mmoja kufaulu na wengine kufeli na kuchukua muelekeo wa suluhisho la pande zote kupata manufaa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alifanya “mazungumzo ya uwazi na yenye tija” pamoja na mwanadiplomasia wa China Wang Yi Alhamisi mjini Jakarta, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje, mfululizo huu wa majadiliano mapya ilisemwa yanalengo la kusimamia tofauti zilizoko kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu.
Marekani na China ziligubika mkutano wa mwaka jana wa ARF, uliofanyika siku chache baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi kuitembelea Taiwan, na kuikasirisha Beijing, ambayo ilianzisha mazoezi ya kijeshi kuzunguka Taiwan na kusimamisha ngazi mawasiliano kadhaa na Washington.
Mkutano wa Alhamisi ni sehemu ya juhudi zinazoendelea kufungua njia za mawasiliano na “kuwajibika kusimamia ushindani kwa kupunguza hatari za dhana potofu na kutotathimini ilivyo,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller alisema katika taarifa.
Wang alimwambia Blinken kitu muhimu katika kurejesha mahusiano kwenye mwelekeo sahihi “ wa busara na mtizamo wa kimaendeleo,” waziri wa mambo ya nje wa China alisema.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters.
Forum