Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:14

Blinken akutana na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China kwenye mkutano wa ASEAN, nchini Indonesia


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Alhamisi amekutana  na mwandiplomasia wa ngazi ya juu wa China Wang Yi pembeni ya mkutano wa Jumuiya ya mataifa ya Asia Kusini Mashariki, ASEAN, nchini Indonesia.

Blinken na Wang walikutana mwezi uliopita mjini Beijing ikiwa sehemu ya juhudi za utawala wa Rais Joe Biden ili kupunguza tofauti zilizopo kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu duniani.

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen aliitembelea Beijing wiki iliyopita muda mfupi baada ya Blinken, wakati mjumbe maalum wa Marekani kuhusu hali ya hewa John Kerry akitarajiwa kwenda China kati ya Julai 16-19.

Blinken na Wang wanashiriki kwenye mkutano wa ASEAN, mjini Jarkata akiwemo pia waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov.

Mkutano huo unaofanyika leo na kesho, Ijumaa unalenga kumaliza mzozo uliopo huko Myanmar pamoja na kupunguza mivutano kwenye bahari ya South China Sea.

Viongozi wa kijeshi wa Myanmar bado hawajatekeleza mpango wa amani walioahidi muda mfupi baada ya kuipindua serikali ya Aung San Suu Kyi mwanzoni mwa 2021.

Forum

XS
SM
MD
LG