Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:58

Viongozi wa Umoja wa ASEAN wakutana Indonesia kusuluhisha migogoro ya kikanda


Viongozi wa Jumuiya ya Mataifa ya Asia Kusini Mashariki wakutana huko Labuan Bajo, Indonesia, Mei 8, 2023.
Viongozi wa Jumuiya ya Mataifa ya Asia Kusini Mashariki wakutana huko Labuan Bajo, Indonesia, Mei 8, 2023.

Rais wa Indonesia Joko Widodo aliuchagua mji wa bandari wa Labuan Bajo kama ni sehemu tulivu kuzungumzia ajenda iliyogubikwa na masuala kadhaa yenye utata.

Hii inajumuisha ghasia za kiraia za umwagaji damu huko Myanmar na kuongezeka kwa mizozo ya kieneo huko South China Sea kati ya viongozi wenza wa Jumuiya ya Mataifa ya Asia Kusini Mashariki.

Kikundi hicho cha kanda chenye nchi 10 mataifa wanachama wanakutana kwa siku tatu kuanzia Jumanne, huku ushindani ukiongezeka kati ya Marekani na China.

Rais wa Marekani Joe Biden amekuwa akiimarisha ushirikiano katika kanda ya Indo-Pacific ili kuidhibiti China kwa uhasimu wake dhidi ya Taiwan na migogoro ya muda mrefu ya kieneo katika eneo la kimkakati la South China Sea ambalo linahusisha wanachama wanne wa Umoja wa ASEAN: Brunei, Malaysia, Ufilipino na Vietnam.

Indonesia, mwenyekiti wa Umoja wa ASEAN mwaka huu, pia imezikabili meli kadhaa za uvuvi za China na walinzi wa pwani kwa kile ambacho Jakarta inasema ilikuwa ni kanda yake binafsi ya kiuchumi inayotambulika kimataifa katika Bahari ya Natuna yenye utajiri wa gesi.

Widodo, ambaye yuko katika mwaka wake wa mwisho katika jukwaa la kimataifa wakati akifikisha ukomo wa awamu zake mbili, alisema ASEAN inalengo la kushirikiana na nchi yoyote kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano.

Hiyo inajumuisha Myanmar ambapo, miaka miwili baada ya jeshi kuchukua madaraka kwa mabavu na kuuondoa utawala wa Aung San Suu Kyi na kuchochea ghasia zilizopelekea umwagaji damu, ASEAN imefeli kudhibiti ghasia hizo katika nchi mwanachama wake.

Mpango wa amani wa nukta tano ulioandaliwa na viongozi wa ASEAN na Jenerali wa Juu wa Myanmar, ambao unataka kusitishwa mara moja mauaji na ghasia nyingine na kuanza kwa mazungumzo ya ngazi ya kitaifa, umepuuzwa na utawala wa kijeshi wa Myanmar.

ASEAN iliacha kuwaalika viongozi wa kijeshi wa Myanmar katika mikutano yake ya nusu mwaka na ikawa inawaruhusu wawakilishi ambao si wanasiasa kuhudhuria. Myanmar imepinga hatua hiyo.

XS
SM
MD
LG