Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:40

Rais wa Indonesia analaani shambulizi huko Myanmar dhidi ya maafisa wa ASEAN


Rais wa Indonesia, Joko Widodo
Rais wa Indonesia, Joko Widodo

Rais Joko Widodo wa Indonesia alisema "Acheni kutumia nguvu, achene ghasia kwa sababu watu ndiyo  wataathirika. Hali hii haitamfanya mtu yeyote ashinde" na kuongeza kuwa Indonesia inawashawishi  wadau wote kufanya mazungumzo na kutafuta suluhu

Rais wa Indonesia Joko Widodo siku ya Jumatatu alilaani shambulizi huko Myanmar dhidi ya maafisa wa ASEAN wanaotoa misaada ya kibinadamu na alitoa wito wa kumalizwa kwa ghasia katika nchi iliyokumbwa na mzozo.

Jokowi, kama rais mwenye umaarufu mkubwa hakutoa maelezo zaidi juu ya tukio hilo lakini alisema halitazuia juhudi za Indonesia na Jumuiya ya mataifa ya Asia Kusini Mashariki (ASEAN) kushinikiza Amani nchini Myanmar. "Acheni kutumia nguvu, achene ghasia kwa sababu watu ndiyo wataathirika. Hali hii haitamfanya mtu yeyote ashinde", alisema na kuongeza kuwa Indonesia inawashawishi wadau wote kufanya mazungumzo na kutafuta suluhu.

Haijajulikana ni nani alihusika na shambulizi hilo. Serikali kivuli ya Umoja wa kitaifa ya Myanmar ambayo inashirikiana dhidi ya wanamgambo wanaopinga utawala wa kijeshi, People’s Defense Forces (PDF) ilisema haikufahamu shambulizi la aina yoyote. PDF haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni yao. Msemaji wa utawala wa kijeshi Myanmar hakujibu ombi la kutoa maoni.

XS
SM
MD
LG