Yoon alikuwa akizungumza katika mkutano kati yake na rais wa Marekani Joe Biden, na waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida, pembeni ya mkutano wa viongozi wa mataifa ya Asia Kusini, ASEAN, unaofanyika Phnom Penh, Cambodia.
Katika mkutano na Biden, Yoon amesisitiza kwamba kuna haja kubwa ya kuimarisha mbinu za kuzuia vitisho vya Korea Kaskazini vinavyoendelea kuongezeka, na kwamba wataionyesha Pyongyang kwamba haitapata faida yoyote kutokana na mpango wake wa nyuklia na makombora.
Korea Kaskazini imekuwa ikifanya majaribio ya kila mara ya makombora, kuwahi kuhsuhudiwa, huku kukiwepo wasiwasi kwamba huenda nchi hiyo inajitayarisha kufanya majaribio ya silaha za nyuklia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2017.