Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:59

Kamala Harris akutana na rais wa Ufilipino Ferdinard Marcos Jr


Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris akiwa kwenye mkutano mjini Manila, Ufilipino.
Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris akiwa kwenye mkutano mjini Manila, Ufilipino.

Makamu rais wa Marekani Kamala Harris Jumatatu amekutana na rais wa Ufilipino Ferdinard Marcos Jr mjini Manila, ili kujadili namna ya kurudisha tena uhusiano mzuri kati ya nchi zao mbili.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuharibika kwa uhusiano wa mataifa yote mawili kwa muda kutokana na masuala ya ukiukaji wa haki za binadamu. Kwa upande mwingine waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd J. Austin na mwenzake wa Indonesia Prabowo Subianto, walikua wanazungumzia juu ya masuala ya kuimarisha ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi zao mbili.

Harris ni afisa wa kwanza wa cheo cha juu wa Marekani kutembelea Manila, tangu rais Ferdinand Marcos kuchukua madaraka mwezi wa June, ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa uhuisano kati ya washirika hawa wa muda mrefu baada ya miaka kadhaa ya uhusiano uliyokua si mzuri chini ya aliyemtangulia Rodrigo Duterte, rafiki wa Bejing.

Alikutana pia na mwenzake wa Ufilipino Sara Duterte,binti ya aliyekua kiongozi wa nchi hiyo, ambae vita vyake vikali vya kupambana na dawa za kulevya vilizusha uchunguzi wa kimataifa kuhusu tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu.

Kwa upande wake Austin amesema kwamba utawala wa Biden ungependa kusaidia Indonesia kushika nafasi muhimu kwenye eneo la Indo Pacific, wakati ukipanua ushirikiano wa kijeshi na taifa hilo. Baadaye wiki hii Austin na Subianto watahudhuria mkutano wa ASEAN wa mawaziri wa usalama utakaofanyikia Cambodia.

XS
SM
MD
LG