Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:12

Makamanda wa Marekani watoa mafunzo ya kijeshi kaskazini mwa Ghana


Wanajeshi wa Ghana wakipewa mafunzo ya kulenga shabaha wakati wa mpango wa kila mwaka wa kukabiliana na ugaidi unaoitwa "Operesheni Flintlock", huko Daboya, Ghana Machi 2, 2023. REUTERS
Wanajeshi wa Ghana wakipewa mafunzo ya kulenga shabaha wakati wa mpango wa kila mwaka wa kukabiliana na ugaidi unaoitwa "Operesheni Flintlock", huko Daboya, Ghana Machi 2, 2023. REUTERS

Makamanda wa Marekani wanaoongoza mazoezi ya kila mwaka ya kukabiliana na ugaidi huko Afrika Magharibi wamezitaka nchi za pwani kushirikiana  ili kudhibiti uasi unaoenea wa Kiislamu badala ya mataifa yasiyo ya Magharibi baada ya Mali mwaka jana kuajiri mamluki wa Russia.

Uhusiano kati ya Russia na Marekani umekuwa wa mvutano zaidi tangu Moscow ilipoivamia Ukraine zaidi ya mwaka mmoja uliopita, Washington na washirika wake wanapinga ushawishi wa Russia huko Afrika Magharibi.

Wakati wa mazoezi ya kijeshi mwezi huu kaskazini mwa Ghana, wakufunzi waliwahimiza wanajeshi kubadilishana nambari za simu na wenzao wa kigeni wanaofanya kazi kwenye mipaka isiyo na alama vizuri, mara nyingi umbali wa maili chache tu kati yao. Kwingineko, wanajeshi hao pia wamejifunza kutumia pikipiki, kama waasi wanavyofanya kwa mwendo wa kasi na ujanja wao.

Ikizidiwa na makundi ya Kiislamu na katikati ya mzozo na wakoloni wao zamani Ufaransa serikali ya kijeshi ya Mali mwaka jana iliajiri wakandarasi binafsi wa kijeshi wa Russia Wagner Group ambao wapiganaji wake wanachukua majukumu muhimu nchini Ukraine kupambana na wanamgambo hao. Hili limetia wasiwasi serikali za Magharibi na Umoja wa Mataifa ambao wanasema hatua hiyo imesababisha kuongezeka kwa ghasia.

XS
SM
MD
LG