Mazoezi hayo pia yanaonekana kuwa sehemu ya kukabiliana na ushirikiano unaoendelea kushamiri kati ya Marekani na washirika wake kutoka eneo hilo.
Stephen Nagy ambaye ni mtaalam wa kiusalama wa kieneo ameiambia VOA kwamba Russia na China wanajaribu kutuma ujumbe kwa Japan na Marekani kwamba hawajafurahishwa na ushirikiano wao kwenye muungano wa NATO, pamoja na kwenye eneo la Indo Pacific, wakati wakilenga kudhihirisha kwamba wanaweza kupata ushirikiano sawa na huo kieneo, sawa na ilivyo kwa Washington na washirika wake.
Kwa upande wa Russia, Nagy ameongeza kusema kwamba zoezi hilo huenda likawa njia ya kuonyesha kwamba bado ina uwezo wa kivita katika ukanda wa mashariki, pamoja na kushawishi mataifa ya Indo Pacific kushirikiana na China katika kukabiliana na Marekani.
Forum