Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:55

Viongozi wa kikabila Namibia wakubali ombi la serikali ya Ujerumani


Heiko Maas
Heiko Maas

Kundi la viongozi wa kikabila kutoka Namibia limesema kuwa limekubali ombi la Ujerumani la kuwalipa fidia pamoja na kukiri kuwa mauaji ya maelfu ya watu yaliyofanyika mwanzoni mwa karne ya 20 yalikuwa ya kimbari.

Wiki iliyopita, Ujerumani ilikubali kuilipa Namibia dola bilioni 1.3 ndani ya kipindi cha miaka 30 kupitia miradi ya maendeleo kuzisaidia jamii za watu waliouawa kati ya mwaka 1904-08.

Hiki ni kipindi ambacho Ujerumani ilikuwa ikitawala taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Ujerumani imeiomba msamaha Namibia kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje Heiko Maas.

Viongozi hao wa kikabila wamesema kuwa wamekubali ridhaa hiyo ingawa kuna nafasi ya kufanya mashauriano zaidi.

Hata hivyo kuna kundi jingine la viongozi wa kikabila lililopinga hatua hiyo likisema kuwa Ujerumani inahitajika kulipa takriban dola bilioni 590 ndani ya kipindi cha miaka 40 pamoja na mfuko wa mafao ya uzeeni kwa jamii zilizoathiriwa.

Wanahistoria wanasema kuwa Jenerali Lothar von Trotha alipotumwa na Ujerumani kuzima uasi kutoka kwa kabila la Herero, aliamuru vikosi vyake kulitokomeza kabila zima.

Zaidi ya watu 65,000 wa kabila la Herero waliuwawa pamoja na wengine 10,000 kutoka kabila la Nama.


XS
SM
MD
LG