Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:13

Ujerumani, Ufaransa na Italia kusitisha chanjo ya AstraZeneca


Ujerumani, Ufaransa, na Italia zimetangaza kusimamisha kutolewa chanjo ya AstraZeneca baada ya ripoti kuonyesha uwezekano wa kuwa na madhara.

Licha ya kuwepo kwa madai ya aina hiyo ya chanjo kuwa na madhara shirika la afya duniani (WHO) linadai kwamba chanjo hiyo ni salama.

Ufaransa, Ujerumani na Italia Jumatatu, zimejiunga na nchi kadhaa wanachama wa Umoja wa Ulaya ambazo zimezuia kutolewa kwa chanjo ya AstraZeneca.

Nchi hizo zimeifuata uamuzi wa Norway ambayo ilitangaza Jumamosi kwamba mtu mmoja alifariki dunia baada ya kupata madhara katika ubongo, na wengine watatu kulazwa baada ya damu kuganda mara tu baada ya kupewa chanjo ya AstraZeneca.

XS
SM
MD
LG