Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:28

Ukoloni : Ujerumani yatambua rasmi mauaji ya kimbari Namibia


Waziri wa Mambo ya Nje Heiko Maas
Waziri wa Mambo ya Nje Heiko Maas

Ujerumani mapema Ijumaa imefikia makubaliano na Namibia kwamba inatambua rasmi mauaji yaliyotokea wakati wa ukoloni yalikuwa ya kimbari.

Kauli hiyo imetolewa wakati taifa hilo likitangaza kutumia dola bilioni 1.3 moja kwenye miradi ya maendeleo nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mashauriano yaliochukua zaidi ya miaka 5 kati ya Namibia na Ujerumani.

Mashauriano hayo yalijikita katika ukatili uliyofanyika kati ya mwaka wa 1904 - 1908 wakati taifa hilo likiwa chini ya ukoloni wa Ujerumani.

Wanahistoria wanasema Jenerali Lothar von Trotha alitumwa na Ujerumani kwenye taifa hilo lililojulakana kama German West Afrika ili kuzima uasi kutoka kwa watu wa kabila la Herero mwaka 1904.

Badala yake Trotha inasemekana kuamuru kutokomezwa kwa kabila hilo lote.

Inasemekana kuwa takriban watu 65,000 kutoka kabila la Herero waliuawa pamoja na wengine 10,000 kutoka kabila la Nama.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema kuwa wameomba msamaha kwa Namibia pamoja na watu wake.


XS
SM
MD
LG