Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:22

Facebook kutoondoa ujumbe wa madai COVID-19 ilitengenezwa


Facebook imesema haitaondoa tena kwenye mtandao wake ujumbe wenye madai Covid-19 ilitengenezwa katika maabara na binadamu.

Kampuni hiyo imesema kuwa hatua hiyo ni kufuatia uchunguzi unaoendelea kuhusiana na kiini cha ugonjwa wa Corona na kwamba imechukuliwa baada ya kushauriana na wataalam wa afya.

Facebook kwa muda sasa imekuwa ikijitahidi kuondoa ujumbe wenye kupotosha kuhusiana na COVID-19 tangu ulipozuka mwaka 2020.

Disemba mwaka uliopita kwa mfano, Facebook ilisema kuwa ingeondoa kila ujumbe uliyokuwa ukipotosha kuhusiana na chanjo za Corona.

Hivi karibuni Rais wa Marekani Joe Biden aliamuru uchunguzi ufanywe ili kubaini chanzo cha virusi vya corona ikiwemo uwezekano kuwa virusi hivyo vilitengenezewa kwenye maabara ya China.

Sasa Facebook imesema kuwa haitaondoa ujumbe wowote unaodai kuwa virusi hivyo huenda vilitengenezwa wakati ikiendelea kushauriana na wataalam wa afya.

Shinikizo linaendelea kote duniani la kubaini iwapo virusi vya corona ni vya kutengenezwa na binadamu.

XS
SM
MD
LG