Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:01

Mkutano wa WHO walenga kukomesha janga la Covid 19 na magonjwa ya milipuko


Mwananmke mmmoja akipokea chanjo ya covid huko East Hollywood Farmer’s Market, Los Angeles, CA.
Mwananmke mmmoja akipokea chanjo ya covid huko East Hollywood Farmer’s Market, Los Angeles, CA.

Kukomesha janga la COVID-19 na kuzuia magonjwa ya milipuko ya baadaye kunatarajiwa kutawala majadiliano wakati wa Mkutano wa 74 wa Afya Duniani wiki hii, chombo kinachofanya maamuzi cha Shirika la Afya Ulimwenguni. Kikao hicho pia kitashughulikia maswala mengine muhimu ya kiafya.

Mkutano huo wa Afya Ulimwenguni wa 2021 utafanyika kwa njia ya mtandao, kuanzia leo Mei 24, 2021 hadi Juni mosi. Hii inakusudia kutuma ujumbe mzito kwamba bado sio salama kwa makundi makubwa ya watu kukusanyika pamoja. Zaidi ya watu 2,750 hadi sasa wamejiandikisha kuhudhuria mkutano huo.

WHO ilitangaza mlipuko wa COVID-19 kuwa janga na dharura ya kimataifa ya afya ya umma, Machi 11, 2020. Tangu wakati huo, kesi za COVID-19 zimeongezeka mara arobaini hadi milioni 162, pamoja na zaidi ya vifo milioni 3.3.

Majadiliano juu ya kile kinachoitwa mkataba wa janga kujiandaa vizuri na kuzuia milipuko ya kuambukiza ulimwenguni inatarajiwa kuchukua hatua kuu katika mkutano huo wa ulimwengu. Afisa mkuu wa sheria wa WHO Steven Solomon anasema kuandaa makubaliano itakuwa mchakato mrefu. Akiongeza kwamba wajumbe hawajaamua ikiwa mazungumzo juu ya mkataba huo yanapaswa kuanza.

Ameongeza kwmba mkutano wa makubaliano ya pamoja ya kisheria yatasimamia yote mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kugawana kwa usawa vitu kama chanjo na upimaji na mifumo.

Mkutano huo utakuwa na ajenda kubwa kuliko zote katika siku nane zijazo na zaidi ya masuala ya kiafya ya kidunia 72 yakichunguzwa. Maswali ya mgao wenye uwiano wa chanjo litakuwa katika majadiliano hayo katika majadiliano haya , nchi tajiri zina mafanikio ya juu katika kuchanja watu wake na kurudi katika Maisha ya kawaida lakini nchi masikini hazifanyi hivyo .WHO inaonya ukosefu wa chanjo wa pamoja unatishia kutomalizika kwa janga na dunia kuondokana na janga hili.

Kama katika miaka iliyopita suala kuipa Taiwan nafasi ya kuwa mwanachama mwangalizi katika mkutano wa WHO utajadiliwa katika kikao cha ufunguzi. China inadai Taiwan kuwa ni kama moja ya majimbo yake na imezuia ushiriki wa Taiwan tangu mwaka 2016 . Sera ya China moja ya Beijing Chama cha Kikomunisti cha China kinasimamia mamlaka juu ya Taiwan.

Mwaka huu, nchi 13 wanachama wa WHO, pamoja na Marekani wametaka Taiwan iruhusiwe kushiriki katika mkutano huo. Wanasema Taiwan ina ufahamu mzuri juu ya kukabiliana na janga hilo na ingekuwa na mengi ya kuchangia. Masuala mengine muhimu yanayopaswa kushughulikiwa ni pamoja na kutokomeza polio, hatua za kasi juu ya upinzani wa antimicrobial kutokufanya kazi na kuzingatia mkakati wa WHO juu ya afya, mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa.

XS
SM
MD
LG