Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:18

Zimbabwe yagundua kesi za kwanza za aina mpya ya virusi vya corona vya India


Makamu rais wa Zimbabwe akiwa katika hospitali ya Wilkins kwa ajili ya chanjo ya kupokea chanjo ya Covid 19.
Makamu rais wa Zimbabwe akiwa katika hospitali ya Wilkins kwa ajili ya chanjo ya kupokea chanjo ya Covid 19.

Zimbabwe imegundua kesi za kwanza za aina mpya ya virusi vya corona ambavo vimeibuka nchini India, Makamu wa Rais Constantino Chiwenga alisema Jumatano, na kuongeza kuwa wasafiri wote kutoka taifa la Asia watalazimika kuwekewa karantini.

Chiwenga, ambaye pia ni waziri wa afya wa Zimbabwe, alisema katika taarifa kesi hizo ziligunduliwa kati ya kundi la watu katika mji wa kati wa Kwekwe baada ya mwanafunzi kurudi kutoka India Aprili 29.

Watu wanaosafiri kutoka au kupitia India watakuwa chini ya karantini ya lazima katika kituo maalum cha karantini na kwa gharama zao, Chiwenga alisema.

Wasafiri kutoka India watafanyiwa vipimo vya COVID-19 wanapowasili hata ikiwa wamepimwa katika nchi yao ya asili.

XS
SM
MD
LG