Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:25

Maafisa wa afya Marekani wanapendekeza kuondoa baadhi ya masharti dhidi ya Corona


Muongozo unaotumika sasa kujilinda dhidi ya COVID-19
Muongozo unaotumika sasa kujilinda dhidi ya COVID-19

Hii inamaanisha hakuna tena kuvaa barakoa au kukaa umbali wa futi sita kati ya mtu hadi mtu katika matukio ya ndani au nje, kulingana na mwongozo uliosahihishwa kutoka kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani (CDC)

Maafisa wa afya Marekani wanapendekeza kuondoa masharti kadhaa ya COVID-19 kwa watu ambao wamepatiwa chanjo kamili dhidi ya virusi hivyo.

Hiyo inamaanisha hakuna tena kuvaa barakoa au kukaa umbali wa futi sita kati ya mtu hadi mtu katika matukio ya ndani au nje, kulingana na mwongozo uliosahihishwa kutoka kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani (CDC). “Ikiwa umepatiwa chanjo kamili unaweza kuanza kufanya shughuli ambazo ulizisitisha, kwa sababu ya janga la Corona”, alisema mkurugenzi wa CDC, Rochelle Walensky.

Dr. Rochelle Walensky, mkurugenzi wa CDC Marekani
Dr. Rochelle Walensky, mkurugenzi wa CDC Marekani

Mkurugenzi wa CDC aliongeza kuwa “sote tumesubiri wakati huu kwa muda mrefu. Kwa sasa barakoa bado zinahitajika kwenye usafiri wa ndege, treni na mabasi”. Walensky alisema CDC itatoa mwongozo mpya hivi karibuni kuhusu masuala ya safari pamoja na mapendekezo kwa shule, kambi, na mipangilio mingine.

Walensky aliwaachia viongozi wa majimbo kuamua ikiwa biashara na sehemu nyingine za mikusanyiko ziendelee kuwataka watu kuvaa barakoa. Idadi ya kesi za COVID-19 pamoja na watu waliopatiwa chanjo katika eneo inapaswa kutoa mwongozo juu ya chaguo hilo, alisema Walensky.

XS
SM
MD
LG