Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:50

Waziri mkuu wa Somalia aahidi uchaguzi wa huru na haki


Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble.
Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble.

Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble alisema alikuwa na nia ya dhati kwa upigaji kura huru na wa haki baada ya kutia saini makubaliano Alhamisi na viongozi kutoka mikoa ya nchi hiyo kufanya uchaguzi usio wa moja kwa moja baada ya uchelewesho kusababisha mzozo.


Chini ya mfumo wa uchaguzi usio wa moja kwa moja, wazee wa koo ndio wanalazimika kuchagua wabunge mwezi Desemba na wabunge wapya watalazimika kumchagua rais mpya mnamo Februari 8. Taratibu zote mbili zilishindikana kutekelezwa, wakati wa mabishano juu ya maswala ambayo ni pamoja na muundo wa tume ya uchaguzi inayosimamia upigaji kura.


Makubaliano hayo yalisababisha wasiwasi kwamba koo zinaweza kugeukiana kila moja na kwamba kundi la al Shabaab lenye mahusiano na al Qaeda wangeweza kutumia ombwe la usalama.


Serikali yangu na mimi tumejitolea kutekeleza uchaguzi huru na wa haki usio wa moja kwa moja. Sote tunawajibika kuhakikisha wanawake wanapata kiwango chao cha asilimia 30 cha nafasi. Ninawashi marais wote wa serikali kuwezesha na kutekeleza hili, Roble alisema baada ya kutia saini makubaliano hayo.


Makubaliano hayo, ambayo yalisomwa kwenye sherehe, yalieleza Roble na majimbo matano ya mikoa watachagua wajumbe wa kamati ya uchaguzi ifikapo Jumapili.


Mkataba huo ulisema uchaguzi usio wa moja kwa moja utafanyika ndani ya siku 60 zijazo, na kila mkoa utachagua maeneo mawili ya kuruhusu wazee wa koo na wawakilishi wa koo kuteuwa wabunge katika bunge kuu.

XS
SM
MD
LG