Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:40

Idadi ya waliofariki shambulizi la bunduki California yafikia tisa

Watendaji wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai FBI wakiwasili katika eneo la Mamlaka ya Usafirishaji ya Santa Clara Valley katika nyumba ya mshukiwa wa mauaji hayo huko San Jose, California, May 26, 2021.
Watendaji wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai FBI wakiwasili katika eneo la Mamlaka ya Usafirishaji ya Santa Clara Valley katika nyumba ya mshukiwa wa mauaji hayo huko San Jose, California, May 26, 2021.

Idadi ya watu waliofariki kufuatia shambulizi la bunduki mjini San Jose, jimbo la California hapa Marekani, imefikia tisa.

Haya yanajiri huku uchunguzi ukiendelea kubaini ni nini kilipelekea mshukiwa, ambaye pia alifariki, kuanza kuwapiga watu risasi kiholela jana asubuhi.

Waathiriwa wanane, ambao walikuwa na umri wa kati ya miaka 29 na 63, walitambuliwa jana Jumatano.

Wa tisa, Alex Ward Fritch, mwenye umri wa miaka 49, alisafirishwa kwenda Kituo cha Matibabu cha Santa Clara, akiwa katika hali mbaya, na aliaga dunia jana jioni.

Shambulizi hilo limefufua mjadala mkali wa kitaifa kuhusu sheria za umiliki wa silaha hapa Marekani

XS
SM
MD
LG