Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:12

Blinken amekamilisha ziara yake mashariki ya kati iliyolenga usitishaji mapigano


Anthony Blinken, waziri wa mambo ya nje wa Marekani
Anthony Blinken, waziri wa mambo ya nje wa Marekani

Waziri Blinken alisifia uongozi thabiti wa mfalme Abdullah wa Jordan katika kusaidia kupatikana amani kati ya Israel na Palestina. Aliongeza kuwa misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza inahitajika hususan maji, usafi wa mazingira na umeme

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alimaliza safari yake ya mashariki ya kati ili kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina katika ukanda wa Gaza, kwa kusifia uongozi thabiti wa mfalme Abdullah wa Jordan katika kusaidia kupatikana amani.

Michango ya hivi karibuni ya Jordan kusaidia kumaliza mzozo nchini Israel inaonyesha jukumu la kudumu la ufalme kama nguvu ya amnai katika eneo hilo ambayo ni moja ya sababu ya uhusiano wetu wenye nguvu na muhimu sana, Blinken aliwaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na mfalme Abdullah huko Amman.

Blinken aliwasili Jordan kituoa cha mwisho ya ziara hiyo kwa mkutano na Mfalme Abdullah ili kuimarisha makubaliano ya usitishaji mapigano. Kuhusu juhudi za kuponya huko Gaza, Blinken alisema jambo la dharura zaidi ni misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza, na hususan maji, usafi wa mazingira, umeme, sote tunapaswa kujumuika pamoja kujibu mahitaji hayo ya haraka. zaidi ya hayo kuijenga tena Gaza.

XS
SM
MD
LG