Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:10

Umoja wa Ulaya wajadili idhinisho la chanjo ya COVID-19


Chanjo ya Pfizer ya kudhibiti COVID-19
Chanjo ya Pfizer ya kudhibiti COVID-19

Maafisa wa Mamlaka ya dawa ya Umoja wa Ulaya, EMA, wanakutana Jumatatu kujadili juu ya kuidhinisha chanjo ya kupambana na virusi vya Corona.

Chanjo hiyo inayojadiliwa ni ile iliyotengenezwa kwa pamoja na kampuni ya BioTech ya Ujerumani na Pfizer ya Marekani.

Hii itakuwa chanjo ya kwanza itakayoidhinishwa kuweza kutumiwa na mataifa yote ya Umoja wa Ulaya.

Mkutano huo wa faragha unafanyika wiki chache baada ya chanjo hiyo kuidhinishwa kwa matumizi ya dharura Uingereza na Marekani.

Na Ikiwa wanasayansi wa EMA wataamua chanjo hiyo ni salama basi maafisa wa mamlaka hiyo mjini Amsterdam wataiidhinisha na kuifahamisha tume ya Ulaya kuchukuwa uamuzi wa kuweza kutumiwa na mataifa 27 wanachama.

Hili litafanyika kabla ya chanjo hiyo kusambazwa katika nchi zote ambapo Ujerumani inasema utaratibu wa kutoa chanjo hiyo utaweza kuanza hapo Disemba 27.

XS
SM
MD
LG