Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:01

EU yaeleza safari ni ndefu kufikia makubaliano ya kibiashara na Uingereza


Meli inayobeba makontena ya MSC Maria Saveria ikiwa inertia nanga katika Bandari ya Felixstowe, mashariki ya Uingereza Disemba 12, 2020. Wakati mazungumzo yanaendelea Brussels juu ya hatma ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya, upungufu wa bidhaa, na bandari ikiwa mzigo iliyokwama.
Meli inayobeba makontena ya MSC Maria Saveria ikiwa inertia nanga katika Bandari ya Felixstowe, mashariki ya Uingereza Disemba 12, 2020. Wakati mazungumzo yanaendelea Brussels juu ya hatma ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya, upungufu wa bidhaa, na bandari ikiwa mzigo iliyokwama.

Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Ursula Von de Leyen amesema Jumatano hawezi kueleza iwapo wataweza kufikia makubaliano ya kibiashara na Uingereza.

Lakini amesema kumekuwepo na maendeleo kwenye mazungumzo na siku zijazo zitakuwa muhimu.

Akizungumza mbele ya bunge la Ulaya amesema maendeleo yamepatikana upande wa biashara lakini matatizo makubwa yamebaki kuhusu suala la uvuvi.

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wanasema wangelipendelea kuona makubaliano ya kibiashara na Uingereza yanafikiwa kabla ya mwisho wa mwaka pale nchi hiyo inapojiondoa rasmi kutoka umoja huo.

Chansela Angela Merkel, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Chansela Angela Merkel, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

Wajumbe wa pande hizo mbili wanaendelea na mazungumzo yao Jumatano juu ya haki za uvuvi Ikiwa ni moja kati ya tatizo kubwa lililobaki na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen anakiri kwamba ingawa inaonekana ni vigumu kufikia makubaliana mnamo siku chache zilizobaki lakini wataendelea kupambana kupata suluhisho.

Rais wa tume ya Ulaya anasema : "Ikiwa kuna njia ya kufikia makubaliano hivi sasa, njia hiyi ni nyembaba sana. Na hivyo jukumu letu ni kujaribu kufikia makubaliano. Habari nzuri ni kwamba tumepata njia ya kuendelea mbele kuhusu masuala kadhaa, lakini tuko katika njia panda yani tukiwa karibu lakini tuko mbali bado juu ya masuala mawili yaliobakia. Moja ni kuhusu masharti ya usawa kwenye biashara na pili suala la uvuvi."

Von dr Leyen anadai siku chache zinazokuja ni muhimu akiwashukuru wabunge wa bunge la Ulaya kwa kuwaunga mkono na kufahamu hali ya mambo yalivyo.

Uingereza inasema makubaliano mapya ya uvuvi yanabidi kuwa chini ya msingi wa kufahamu kwamba maeneo ya mipaka ya uvuvi ya Uingereza ni kwa ajili ya maboti ya wavuvi wa Uingereza kwanza.

Lakini Umoja wa Ulaya unataka kupewa nafasi ya maboti yao kuingia kwenye maeneo hayo chini ya makubaliano ya kuridhiana kuhusiana na uvuvi kwa ujumla kama sharti la awali katika makubaliano ya biashara huru. Kwa hivyo ingawa uvuvi ni sehemu ndogo sana katika uchumi wa pande zote mbili lakini unauzito mkubwa wa kisiasa.

Uingereza haitokuwa tena mwanachama wa EU hapo Januari mosi lakini italazimika kufuata kanuni na umoja huo hadi mwisho wa mwaka 2020.

Hiyo ina maana kila nchi inahaki ya kuingia katika eneo la mwengine kama ilivyo hivi sasa, lakini hawawezi kuvua namna wanavyotaka. Hivyo suala linajitokeza ni kiasi gani cha samaki kila upande unabidi kuvua? Msemaji wa kamisheni ya EU, Daniel Ferrie, anasema pande zote mbili zinahitaji kufikia makubaliano kwanza kabla ya mwaka kumalizika.

Daniel Ferrie anatema : "Tumekubaliana kuendelea zaidi na mazungunzo juu ya mustakbal wa ushirikiano wetu na Uingereza. Ingawa tuko katika siku za mwisho tunadhani ni wajibu wetu , na ni jambo la busara kuendelea na majadiliano. Tuna fahamu bila shaka hatuna muda wa kutosha kuweza kufikia makubaliano hapo Januari mooi lakini tutajitahidi.

Wakishindwa kufikia makubaliano basi inamaanisha ushuru na kodi zitapanda na usafirishaji wa bidhaa kati ya pande mbili utakuwa ghali zaidi.

XS
SM
MD
LG