Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:06

Wananchi Uingereza waanza kupiga kura


Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akizungumza bungeni.
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akizungumza bungeni.

Wapiga kura nchini Uingereza wameanza kupiga kura mapema Alhamisi kwenye uchaguzi mkuu wa mapema ambao huenda ukaleta suluhisho lililosubiriwa kwa muda mrefu kwenye mgogoro kuhusu kujiondoa kwa taifa hilo kwenye Umoja wa Ulaya (EU), hatua iliyoidhinishwa kupitia kura ya maoni 2016.

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amelenga kampeni yake kwa kauli mbiu ya 'Get Brexit Done', amesema kuwa iwapo chama chake cha Conservative kitapata wingi kwenye bunge, basi ataweza kishinikiza mkataba wa Brexit uliokataliwa awali na kuhakikisha kuwa Uingereza inajiondoa kwenye Umoja wa Ulaya ifikapo Januari 31.

Mpinzani wake mkuu kutoka chama cha Labor, Jeremy Corbyn amesema kuwa iwapo atashinda, Uingereza itaitisha kura nyingine ya maoni ili wakazi waamue iwapo bado wanataka kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya, au wabaki miongoni mwa mataifa 28 wanachama. Johnson alichukua madaraka mwezi Julai baada ya mtangulizi wake.

XS
SM
MD
LG