Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:26

Umoja wa Afrika waadhimisha miaka 60 ya kumbukumbu za Siku ya Afrika


Siku ya Furaha Afrika: Maadhimisho ya Miaka Sitini ya kumbukumbu za Siku ya Afrika
Siku ya Furaha Afrika: Maadhimisho ya Miaka Sitini ya kumbukumbu za Siku ya Afrika

Umoja wa Afrika Alhamisi umeadhimisha miaka 60 ya kumbumbuku za Siku ya Afrika, wakati ikitangaza Eneo Huru la Biashara ya Barani Afrika, makubaliano ya viongozi wa kiafrika kwa uchumi wa bara hilo. 

Mkataba wa AfCTA uliosimamiwa na AU ulisainiwa nchini Rwanda na nchi 44 za Afrika mwaka 2018 ili kuimarisha biashara ndani ya bara hilo. Tangu wakati huo, nchi 54 za Afrika, ukiitoa Eritrea, zimesaini makubaliano hayo, na kuongeza wigo wa mkataba huo.

Jukwaa la Kibiashara la AfCTA
Jukwaa la Kibiashara la AfCTA

Achaleke Christian Leke, balozi wa vijana wa AU kwa ajili ya amani kwya Afrika ya Kati, ameiambia VOA kuwa AfCFTA itaisaidia Afrika kunufaika na rasilimali zake, bidhaa zenye ubunifu na soko la Afrika.

“Hata katika nchi ambapo wameendelea ( huko Afrika), nchi nyingine za Kiafrika haziwezi kunufaika nafikiri ndio maana fikra hii tukufu ya ukanda huru wa biashara Afrika ni muhimu sana na imekuja wakati muafaka,” Leke alisema.

Sekretarieti ya AfCFTA inakadiria kuwa muungano wa biashara huru wa kiwango cha dola za Marekani trilioni 3.4 unaweza kufikiwa miongoni mwa watu bilioni 1.3 Afrika.

AfCFTA inasema mkataba wa biashara una uwezo wa kuwanyanyua kimaisha watu milioni 30 kutoka katika lindi la umaskini huku ukipandisha viwango vya mapato kufikia dola za Marekani bilioni 450 ifikapo 2035.

Mkutano wa AU Ethiopia Feb 18, 2023.
Mkutano wa AU Ethiopia Feb 18, 2023.

Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) imezitaka nchi za Kiafrika kutekeleza mkataba wa eneo huru la biashara, likisema itatoa msukumo mkubwa kwa uzalishaji katika uchumi wa Afrika na kusaidia kutatua changamoto kama vile mabadiliko ya hali ya hewa.

Lakini wataalam kadhaa wanadai kuwa AfCFTA inaweza kuwa inaelekea kufeli iwapo viongozi wa Afrika hawatatua changamoto zilizopo katika bara hilo kama vile ufisadi uliokithiri na miundombinu mibovu. Leke anakubaliana nayo, lakini anatoa angalizo kuwa mkataba huo unahitaji kutekelezwa.

Forum

XS
SM
MD
LG