Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:14

Hatimaye Afrika yajitosa kwenye tasnia ya anga



Roketi ya SpaceX Starship ikiwa Boca Chica, Texas. Picha na Patrick T. Fallon / AFP.
Roketi ya SpaceX Starship ikiwa Boca Chica, Texas. Picha na Patrick T. Fallon / AFP.

Baada ya miongo kadhaa kutoshiriki kwa nchi za Kiafrika, sasa zinajitosa katika tasnia ya anga, zikitumaini kupata mafanikio katika kilimo, kuzuia majanga na usalama.

Ivory Coast, ambayo hivi karibuni ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa "NewSpace Africa" ulioandaliwa na Umoja wa Afrika, imetangaza kuundwa kwa idara ya anga na ina mipango ya kujenga satelaiti ya kwanza ya nano nchini humo ifikapo mwaka 2024.

Mwezi Aprili, satelaiti ya kwanza kufanyakazi ilikuwa ya Kenya ambayo iliwekwa kwenye obiti na roketi ya SpaceX ambayo ilirushwa kutokea Marekani.

Nchi hizo mbili zinafuata nyayo za nchi chipukizi ikiwemo Afrika Kusini, Nigeria, Algeria na Misri – nchi za mwanzo kumiliki satelaiti ya kwanza ya Kiafrika iliyotumwa angani mwaka 1998.

Kulingana na mratibu wa progamu ya anga wa AU Tidiane Ouattara, takriban nchi 15 za Afrika zina idara za anga.

Mwaka 2018, AU ililisaidia shirika la Anga la Afrika, ambalo makao yake makuu yatakuwa Cairo likiwa pamoja na Shirika la Anga la Misri, ili kuhamasisha uratibu miongoni mwa wanachama wa AU.

Kwa mujibu wa baraza la ushauri la shirika lisilo la kiserikali la Space Generation lenye makao yake mjini Vienna, nchi za Afrika zimerusha satelaiti 41 tangu mwaka 2016, zikiongozwa na Misri, Afrika Kusini, Algeria na Nigeria.

Satelaiti pia zinaweza kuchukua jukumu la kiusalama, kufuatilia uporaji wa kigeni wa uvuvi wa katika maeneo ya pwani na mienendo ya waasi wanajihadi wanao sababisha vurugu katika eneo la Sahel na kaskazini mwa Msumbiji.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG