Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:58

Serikali ya Kenya imewaondoa raia wake kutoka Sudan


Raia wa Kenya wakiwasili nchini mwao kutoka Sudan
Raia wa Kenya wakiwasili nchini mwao kutoka Sudan

Wazazi wenye khofu wa wanafunzi wa wakenya walioko katika chuo kikuu nchini Sudan wamekuwa wakifika kwenye ofisi ya kaunti ya Wajir nchini Kenya wakati wakisubiri kwa habari kuhusu watoto wao waliokwama katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum

Serikali ya Kenya imewaondoa raia wake kutoka Sudan iliyokumbwa na mzozo; lakini sitisho tete la mapigano ambalo limewekwa linafikia mwisho Jumapili usiku, wazazi wa wanafunzi wa Kenya ambao walikwama nchini Sudan waliiomba Nairobi kuharakisha mchakato wa kuwaondoa. Wanafunzi wengi ni kutokea kaunti ya Wajir.

Wazazi wenye khofu wa wanafunzi wa wakenya walioko katika chuo kikuu nchini Sudan wamekuwa wakifika kwenye ofisi ya kaunti ya Wajir nchini Kenya wakati wakisubiri kwa habari kuhusu watoto wao waliokwama katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Huku sitisho tete la mapigano likiwa limewekwa kati ya pande zinazopigana nchini Sudan, wazazi wengi walioko nchini Kenya wana wasi wasi mkubwa kuhusu usalama wa watoto wao, akiwemo Osman Mohamed.

“Mtoto wangu wa kiume ni miongoni mwa wale ambao wamekwama katika chuo kikuu, na amenithibitishia kwamba kuna wengine kadhaa ambao wanasubiri mawasiliano kutoka ubalozini, na baod hawajapata habari yoyote,” amesema Mohamed.

Kundi la kwanza la wakenya waliondolewa huko limewasili kwa ndege ya jeshi la anga la Anga kutokea Sudan Kusini ni kiasi tu cha wiki moja iliyopita baada ya mapigano kuanza. Kundi la watu 39, wakiwemo wanafunzi wa Kenya 19, waliondolewa kufuatia ghasia katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ambazo zilipelekea mamia ya vifo.

Abdi Hamza mmoja wanafunzi wa afya katika International University of Africa katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum alizungumza na mwandishi wa habari na kuelezea hali ilivyokuwa, “tulianza safari yetu siku mbili zilizopita kutoka Khartoum, tulifika kwa basi huko Kosti karibu na mpaka, halafu kutoka Kosti tuliwkenda Jodah. Huko Jodah tulipokelewa na serikali ya Sudan Kusini,” aliongezea Hamza.

Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Aden Duale aliwaambia wana habari wakati akiwapokea wakenya hao kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi kwamba Kenya ina nia ya dhati ya kuhakikisha usalama wa raia wake wote waliokwama nchini Sudan.

“Tutahakikisha kwamba ndege zote na mipango ya usafiri inakuwepo kwa kuwaondoa wakenya wote. Kuna zaidi ya wakenya 3,000 ambao wako nchini Sudan, na hadi hivi sasa, tumeweza kuwatoa wakenya 900 katika sehemu mbali mbali za Khartoum na Sudan kwa jumla,” alisema waziri Duale.

Licha ya juhudi za serikali ya Kenya, wazazi wa wanafunzi hao ambao bado wako nchini Sudan wameelezea khofu yao kuhusu wanafunzi waliokwama katika mapigano na kuiomba serikali kuwaondoa haraka sana.

Mohamed anasema wanaiomba sana serikali kuharakisha mchakato wa kuwaondoa ili walau kabla ya muda wa sitisho la mapigano haujakwisha, iwe wanafunzi wote walioko Khartoum, wamesafirishwa kwenda sehemu salama.”

Wizara ya mambo ya nje ya Kenya mapema wiki hii iliwaambia wanafunzi wa Kenya kujiandikisha kwenye ubalozi wao mjini Khartoum katika juhudi ya kuharakaisha mchakato wa kuwaondoa.

Hakuna safari zaidi za ndege kwa wakenya kutoka Sudan.

Ahmed Amdey mtafiti wa elimu mjini Nairobi anasema “ukweli ni kwamba hatuwezi kuelezea watu 2,000 pamoja na wanafunzi wetu na hili linatia wasi wasi kwasababu tunazungumzi watu 3,000; ni 900 tu wameweze kupatikana na kuondolewa, hiyo inaacha idadi kubwa zaidi ambayo haijashughulikiwa. Pili, ukweli ni kwamba kati ya hao 900 ambao wametajwa waliwea tu kuwaondoa 35, inaonyesha jinsi juhudi ndogo zilizopo huko. Nadhnai serikali ya Kenya inaweza kufanya vizuri zaidi.”

Mapigano kati ya majeshi ya Sudan na kundi hasimu la kijeshi la Rapid Support Forces yamechochea kuharakishwa kuondolewa kwa maelfu ya raia wa kigeni.

Huku sitisho tete la mapigano likiwa limewekwa, wazazi wengi wakenya kama Osman Mohamed wanakhofia wapendwa wao—lakini wamewekwa matumaini kuwa watarejea nyumbani kwa salama.

((Imetayarishwa na Ahmed Hussein, VOA News, Wajir, Kenya))

XS
SM
MD
LG