Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:51

Shambulizi la anga linaloshukiwa kufanywa na Israel limewajeruhi raia huko Syria


Mfano wa mashambulizi yanayoshukiwa kufanywa na Israel kwa Syria
Mfano wa mashambulizi yanayoshukiwa kufanywa na Israel kwa Syria

Israel imefanya mamia ya mashambulizi ya anga katika eneo la Syria kwa miaka mingi ikilenga vikosi vinavyoungwa mkono na Iran, wapiganaji wa Hezbollah wa Lebanon na maeneo ya jeshi la Syria

Shambulizi la anga linaloshukiwa kufanywa na Israel karibu na mji wa Syria wa Homs liliwajeruhi raia watatu na kusababisha moto katika kituo kimoja cha mafuta cha raia Jumamosi, kulingana na SANA, shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Syria.

Israel imefanya mamia ya mashambulizi ya anga katika eneo hilo kwa miaka mingi, kwa ujumla ikilenga vikosi vinavyoungwa mkono na Iran, wapiganaji wa Hezbollah wa Lebanon na maeneo ya jeshi la Syria.

Israel kwa kawaida haitoi maelezo yoyote kuhusu shughuli zake katika eneo hilo, lakini imesema kuwa haitamruhusu adui wake mkuu Iran kuanzisha harakati zozote nchini Syria.

Shirika linalofuatilia haki za binaadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza limeripoti kwamba wanajeshi wanne wa Syria walijeruhiwa katika shambulio hilo na kwamba milipuko mikubwa ilisikika wakati mabomu yakilipuliwa.

XS
SM
MD
LG