Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:46

Mapigano makali yanaendelea kuripotiwa Sudan


Hali ilivyo kufuatia mapigano mjini Khartoum nchini Sudan. April 25, 2023.
Hali ilivyo kufuatia mapigano mjini Khartoum nchini Sudan. April 25, 2023.

Vikosi vya jeshi vilipambana na wanajeshi mjini Khartoum wakati uhasama mkubwa uliosababisha vifo ukiingia wiki ya tatu licha ya sitisho la mapigano hivi karibuni ambao ulipangwa kumalizika rasmi mwishoni mwa siku.

Mapigano makali yameutikisa mji mkuu wa Sudan Jumapili wakati maelfu ya watu wakikimbia vurugu hizo za umwagaji damu ambapo Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan Abdallah Hamdok ameonya kuhusu hatari ya mapigano kutumbukia katika vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.

Vikosi vya jeshi vilipambana na wanajeshi mjini Khartoum wakati uhasama mkubwa uliosababisha vifo ukiingia wiki ya tatu licha ya sitisho la mapigano hivi karibuni ambalo lilipangwa kumalizika rasmi mwishoni mwa siku.

"Kumekuwepo mapigano makali na milio ya risasi ilisikika tangu asubuhi katika mtaa wangu", mkazi mmoja wa kusini mwa Khartoum aliliambia shirika la habari la AFP.

Mapigano yaliripotiwa kuzunguka makao makuu ya jeshi katikati mwa Khartoum na jeshi pia lilifanya mashambulizi ya anga katika mji pacha wa mji mkuu wa Omdurman katika Mto Nile.

Mataifa ya kigeni yamekuwa yakihangaika kuwahamisha maelfu ya raia wao kwa njia ya anga, barabara na bahari tangu mapigano hayo yalipoikumba Sudan, April 15 katika nchi iliyo maskini na dhaifu kisiasa.

Ndege ya kwanza ya Shirika la Msalaba Mwekundu ilipeleka tani nane za misaada ya kibinadamu kwenda Port Sudan kutokea Jordan leo Jumapili. Ilibeba vifaa vya matibabu ili kuwasaidia wagonjwa 1,500 Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imesema.

XS
SM
MD
LG