Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:50

Wizara ya ulinzi Uingereza yatoa tathmini ya mashambulizi ya Russia nchini Ukraine


Mfano wa majengo huko Ukraine yalivyoharibiwa kutokana na uvamizi wa Russia
Mfano wa majengo huko Ukraine yalivyoharibiwa kutokana na uvamizi wa Russia

Wimbi la mashambulizi lilihusisha makombora machache kuliko yale ya msimu wa baridi na haionyeshi kuwa yalikuwa yakilenga miundombinu ya nishati ya Ukraine, wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema.

Mashambulizi ya makombora ambayo Russia iliyarusha dhidi ya Ukraine Ijumaa yanaashiria Russia inaachana na matumizi ya mashambulizi ya masafa marefu, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi katika taarifa yake ya kila siku ya kijasusi iliyochapishwa kwenye Twitter, kuhusu uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Wimbi la mashambulizi lilihusisha makombora machache kuliko yale ya msimu wa baridi na haionyeshi kuwa yalikuwa yakilenga miundombinu ya nishati ya Ukraine, wizara hiyo ilisema. Kuna uwezekano wa kweli kwamba Russia ilikuwa ikijaribu kuviingilia kati vitengo vya akiba vya Ukraine na vifaa vya kijeshi vilivyotolewa hivi karibuni kwa Ukraine.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema Russia inaendesha mchakato usio na tija wa kulenga na kuweka kipaumbele kwa umuhimu wa kijeshi badala ya kuzuia uharibifu ikiwa ni pamoja na vifo vya raia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alitumia hotuba yake kwa njia ya video Ijumaa usiku kulaani mashambulizi makubwa ya anga ya Russia ya kwanza ya kiwango kikubwa kufanyika katika miezi kadhaa.

XS
SM
MD
LG