Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:14

Guterres anawasihi viongozi wa Afrika kuzidisha juhudi za kuleta amani DRC


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Guterres alihutubia mkutano wa ngazi ya juu nchini Burundi wa mataifa ya Afrika ambayo yalitia saini makubaliano ya Umoja wa Mataifa mwaka 2013 kwa ajili ya kuhamasisha utulivu na usalama katika taifa hilo lenye utajiri wa madini, lakini limegubikwa na mzozo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Jumamosi aliwasihi viongozi wa Afrika kuzidisha juhudi zao za kuleta amani huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mahala ambako makundi yenye silaha yamekwua yakiwatisha raia kwa miongo kadhaa.

Guterres alihutubia mkutano wa ngazi ya juu nchini Burundi wa mataifa ya Afrika ambayo yalitia saini makubaliano ya Umoja wa Mataifa mwaka 2013, kwa ajili ya kuhamasisha utulivu na usalama katika taifa hilo lenye utajiri wa madini, lakini limegubikwa na mzozo.

Alisema makubaliano yaliyoanzishwa muongo mmoja uliopita yaliashiria mabadiliko ya ushirikiano katika eneo linalokumbwa mara kwa mara na matatizo, lakini mgogoro uliopo sasa unaelezea namna tunavyopaswa kusonga mbele.

Licha ya juhudi zetu za pamoja, zaidi ya makundi mia moja yenye silaha yaliyopo ndani ya congo na nje bado yanaendesha harakati hivi leo na hivyo kutishia uthabiti wa eneo zima la Maziwa Makuu, Guterres aliuambia mkutano wa marais na viongozi waandamizi wengine akiwa mjini Bujumbura.

XS
SM
MD
LG