Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:18

Marais sita wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Ukraine


Jengo la ghorofa likiwaka moto katika jiji la Bakhmut. Picha na Kitini / Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine / AFP.
Jengo la ghorofa likiwaka moto katika jiji la Bakhmut. Picha na Kitini / Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine / AFP.

Ujumbe wa viongozi nchi sita kutoka barani Afrika unatarajiwa kufanya mazungumzo na Kyiv pamoja na Moscow yenye lengo la "kuanzisha mchakato wa amani."

Viongozi hao pia watazungumzia suala gumu la jinsi vikwazo vya Russia vinaweza kulipiwa na bei kubwa za mbola ambayo inaipeleka barani Afrika, mpatanishi mkuu ambaye ataendesha mazungumzo hayo alisema katika mahojiano na shirika la habari laAssociated Press.

Jean-Yves Ollivier ni mpatanishi wa kimataifa ambaye amekuwa akifanya kazi kuandaa mazungumzo hayo kwa kipindi cha miezi sita, alisema viongozi hao wa Afrika pia watajadili suala linalohusiana na kurahisisha upitishaji zaidi wa nafaka kutoka Ukraine wakati wa vita na uwezekano wa kubadilishana wafungwa, mfasara huo katika nchi zote mbili umetajwa kama mkakati wa amani.

Mazungumzo yanaweza kufanyika mwezi ujao, Ollivier alisema.

Ollivier aliwasili mjini Moscow siku ya Jumapili na pia atakwenda Kyiv kwa mikutano na maafisa wa ngazi ya juu ili kuweka "mipango" kwa ajili ya mazungumzo yatakayofuata. Wakati mapigano yanaendelea marais hao sita wa Afrika huenda watasafiri hadi Kyiv kwa treni usiku kutoka Poland, alisema mpatanishi huyo.

Katika nyakati tofauti, rais wa Russia Vladimir Putin na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wote wamekubali kuwa wenyeji wa ujumbe huo wa maraisi kutoka Afrika Kusini, Senegal, Misri, Jamhuri ya Congo, Uganda na Zambia.

Mazungumzo hayo pia yanaungwa mkono na Marekani, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na China, Ollivier alisema katika mazungumzo kwa njia ya video na shirika la habari la AP siku ya Ijumaa.

Hakuna upande unaoonekana kuwa tayari kuacha mapigano.

Mazungumzo hayo yalitangazwa wiki iliyopita na rais wa Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa wakati Russia ilipoanzisha mashambulizi makali ya anga dhidi ya Kyiv.

Siku ya Jumapili, Russia ilidai kuuteka mji muhimu wa Bakhmut uliopo mashariki mwa Ukraine madai ambayo yamekanushwa na Ukraine.

XS
SM
MD
LG