Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:22

Uharibifu mkubwa zaidi waripotiwa Bakhmut, mji wa Ukraine uliodumu kwa miaka 400


Picha inayoonyesha hali mjini Bakhmut
Picha inayoonyesha hali mjini Bakhmut

Mapigano ya miezi tisa ya Bakhmut, yameharibu mji huo  wa mashariki mwa Ukraine ambao umekuwepo kwa miaka 400 na kuua darzeni za maelfu ya watu, huku Ukraine ikitumia mkakati ulionuiwa  kulichosha jeshi la Russia, Shirika la habari la AP limeripoti.

Ukungu uliosababishwa na mashambulizi uliifanya vigumu kuthibitisha hali ilivyokuwa Jumapili, katika vita virefu zaidi tangu uvamizi wa Russia kuanza nchini Ukraine, huku wizara ya ulinzi ya Russia ikiripoti kwamba kikosi cha kibinafsi cha Wagner, kikisaidiwa na wanajeshi wa Russia, kilikuwa kimeuteka mji huo.

Licha ya yote hayo, mji huo mdogo, kwa muda mrefu umekuwa ni wa kuonyesha taswira ya kiishara zaidi kuliko thamani yake ya kimkakati kwa pande zote mbili, kwa mujibu wa wachambuzi.

Kigezo cha kweli zaidi, cha mafanikio kwa vikosi vya Ukraine, kimekuwa uwezo wa wanajeshi wake kuvizuia vikosi vya Russia.

AP inaripoti kwamba jeshi la Ukraine limelenga kumaliza rasilimali na kuwavunja moyo wanajeshi wa Russia katika eneo dogo, lakini muhimu, la kilomita 1,500, huku Ukraine ikijiandaa kwa mashambulio makubwa ya kulipiza kisasi, katika vita hivyo vilivyodumu kwa miezi 15.

XS
SM
MD
LG