Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:13

Mwandishi wa habari wa AFP auawa kwa roketi nchini Ukraine


Mwandishi wa habari wa AFP Arman Soldin, apiga selfie akiwa kazini nchini Ukraine. Aliuawa kwa shambulio la roketi, Mei 9, 2023
Mwandishi wa habari wa AFP Arman Soldin, apiga selfie akiwa kazini nchini Ukraine. Aliuawa kwa shambulio la roketi, Mei 9, 2023

Mwandishi wa shirika la habari la AFP nchini Ukraine anayesimamia kazi ya kupiga video Arman Soldin aliuawa Jumanne na roketi iliyorushwa karibu na mji wa Chasiv Yar mashariki mwa Ukraine, waandishi wa AFP na walioshuhudia tukio hilo walisema.

Shambulio hilo lilifanyika saa kumi na nusu alasiri majira ya huko katika kitongoji cha mji uliokaribu na Bakhmut, kitovu cha mapigano mashariki mwa Ukraine kwa miezi kadhaa.

Timu ya waandishi wa AFP ilishambuliwa kwa roketi wakati wakiwa pamoja na wanajeshi wa Ukraine.

Soldin, mwenye umri wa miaka 32, aliuawa wakati roketi ilipopiga karibu na mahali alipokuwa amelala.

Wanahabari wenzake hawakujeruhiwa.

“Shirika lote limesikitishwa kwa kumpoteza Arman,” mwenyekiti wa AFP Fabrice Fries alisema.

Amesema “Kifo chake ni ukumbusho wa kutisha wa athari za hatari wanazokabiliana nazo waandishi wa habari kila siku wakiripoti mzozo wa Ukraine.”

Soldin alikuwa raia wa Ufaransa, ambaye alizaliwa Sarajevo.

XS
SM
MD
LG