Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:29

Kundi la G7 lazidisha shutuma dhidi ya China


Rais wa Marekani Joe Biden alipowasili kukutana na viongozi wengine wa G7 huko Hiroshima, magharibi mwa Japan, Ijumaa.AP
Rais wa Marekani Joe Biden alipowasili kukutana na viongozi wengine wa G7 huko Hiroshima, magharibi mwa Japan, Ijumaa.AP

Kundi la nchi saba zenye nguvu za kiviwanda duniani Jumamosi lilizidisha shutuma zake dhidi ya kuongezeka kwa vitisho vya usalama vya kijeshi na kiuchumi vya China.

Wakati huo huo wakiisihi Beijing kuishinikiza Russia kuacha uchokozi wake wa kijeshi na kuondoa wanajeshi wake kutoka Ukraine.

Katika taarifa ya pamoja ya mkutano wao wa G7 huko Hiroshima, kundi hilo liliikosoa China kwa kutumia mbinu ya ‘kulazimisha kiuchumi’, kuweka jeshi katika huko South China Sea na harakati zake za kuingilia kati zenye lengo la kudhoofisha usalama wa wanadiplomasia, uadilifu wa taasisi za kidemokrasia na ustawi wa kiuchumi. .

G7 waliapa tena kuiunga mkono Ukraine kwa muda wote bila kujali itachukua muda gani katika kukabiliana na vita haramu vya uvamizi wa Russia.

XS
SM
MD
LG