Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:25

Zelensky akanusha madai ya Russia kwamba 'imeuteka kabisa' mji wa Bakhmut


Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema mwishoni mwa mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri zaidi duniani G-7, mjini Hiroshima, Japan, kwamba Russia haikuwa imeuteka kabisa mji wa Bakhmut kama alivyodai Rais Vladmir Putin.

Hata hivyo, Zelensky aliongeza kuwa kuharibiwa kabisa kwa mji wa Bakhmut na vikosi vya Russia, kutaleta kumbukumbu ya shambulio la Hiroshima mwishoni mwa vita vya pili vya dunia.

"Hiroshima ni jiji lililojengwa upya sasa. Na tuna ndoto ya kujenga upya miji yetu yote ambayo sasa ni magofu, na kila kijiji ambacho, hakuna nyumba moja iliyobaki, baada ya mashambulizi ya Russia," Zelenskyy alisema Jumapili.

Rais huyo alionya kwamba ikiwa ulimwengu hautaungana dhidi ya mvamizi wa Russia, itakuwa "suala la muda tu kabla ya wahalifu wengine kutaka kuanzisha vita kama hivyo," na kuongeza kwamba, alikuwa mjini Hiroshima ili ulimwengu usikie wito wa Ukraine wa kuungana pamoja kutoka huko.

Zelenskyy alikanusha madai ya Russia kwamba ilikuwa imeutwaa mji wa Bakhmut. Siku ya Jumamosi, Russia ilisema imeuteka mji huo uliokumbwa na msukosuko baada ya vita vilivyodumu kwa miezi tisa huko, ambavyo vinatajwa kama vilivyosababisha umwagikaji wa damu zaidi, tangu vita vya pili vya dunia.

Rais wa Russia Vladimir Putin aliwapongeza wanajeshi wake, na vikosi vya Wagner, kwa kile alichokiita ushindi, ambao ulipingwa na Kyiv, ambayo ilisema bado inashikilia sehemu ndogo ya mji wa mashariki.

XS
SM
MD
LG