Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:08

Bashar al Assad amehutubia Umoja wa Nchi za Kiarabu baada ya kuondolewa 2011


Rais wa Syria Bashar al-Assad
Rais wa Syria Bashar al-Assad

"Mkutano wa umoja wa nchi za kiarabu ni fursa ya kihistoria kuelezea masuala ya kieneo bila ya uingiliaji  wa kigeni, ambapo inatufanya sisi tujitafakari tena katika dunia ambayo inaundwa hii leo, kwa ajili ya sisi kuwa na jukumu lililo hai", aliongeza Assad

Ni mara ya kwanza kwa Rais wa Syria Bashar al Assad anahutubia chombo hicho tangu Syria ilipoondolewa kutoka Umoja wa nchi za kiarabu mwaka 2011 kufuatia ukamataji wake alioufanya kwa waandamanaji wanaompinga ndani ya Syria.

Mkutano wa umoja wa nchi za kiarabu ni fursa ya kihistoria kuelezea masuala ya kieneo bila ya uingiliaji wa kigeni, ambapo inatufanya sisi tujitafakari tena katika dunia ambayo inaundwa hii leo, kwa ajili ya sisi kuwa na jukumu lililo hai, aliongeza Assad.

Mmoja baada ya mwingine, viongozi wa kiarabu walikaribisha kurudi kwa Syria kwenye umoja wan chi za kiarabu na katika hotuba yake mwenyewe Assad alirudia akisema kwamba Syria ni mtoto wa dunia ya kiarabu.

Lakini kiongozi mmoja muhimu hakusikika akiongea, Emir Tamim bin Hamad al Thani wa Qatar ambaye mwaka 2018 alimuita rais wa Syria mualifu wa vita. Wakati huo huo akitafuta uungaji mkono kwa watu wake, Rais wa Ukraine Volodymir Zelenskyy pia alihudhuria mkutano huo, wakati mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman alipoelezea utayari wake wa kuongoza mazungumzo ya vita kati ya Moscow na Kyiv.

XS
SM
MD
LG