Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:20

Rais wa Ukraine anaungana na viongozi wa G7 nchini Japan


Rais wa Ukraine, Volodymy Zelenskyy
Rais wa Ukraine, Volodymy Zelenskyy

Uthibitisho wa Zelenskyy kuhudhuria umekuja wakati viongozi wa G-7 kutoka Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Uingereza, Japan na umoja wa ulaya wakirudia tena nia yao ya dhati ya kusimama pamoja dhidi ya hatua isiyo halali ya Russia, vita vya uchokozi dhidi ya Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymy Zelenskyy ataungana na viongozi wa kundi la mataifa tajiri G-7 huko Hiroshima nchini Japan, safari ndefu ya Zelenskyy kutoka nchi yake iliyokumbwa na vita wakati wanachama wa G-7 wanaahidi kuleta ushirikiano kamili na amani ya kudumu nchini Ukraine.

Zelenskyy alitarajiwa kulihutubia kundi hilo kwa njia ya viedo Jumapili lakini waziri wa ulinzi na usalama wa kitaifa wa Ukraine, Oleksiy Danilov akizungumza kwenye televisheni ya taifa alithibitisha kwamba Zelenskyy atahudhuria mkutano huo.

"Masuala muhimu sana yataamuliwa huko na kwa hivyo basi uwepo kamili wa rais wetu kwa hakika ni muhimu sana kwa ajili ya kutetea maslahi yetu", alisema.

Uthibitisho wa Zelenskyy kuhudhuria umekuja wakati viongozi wa G-7 kutoka Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Uingereza, Japan na umoja wa ulaya wakirudia tena nia yao ya dhati ya kusimama pamoja dhidi ya hatua isiyo halali ya Russia, vita vya uchokozi dhidi ya Ukraine.

XS
SM
MD
LG