Wakati hofu hiyo ikiongezeka mpaka unaotenganisha Uturuki na Iran umekuwa ni mfano wa kuzuka mzozo huo.
Shirika la habari la AP linaripoti kwamba uzio kati ya nchi hizo mbili una nafasi ya uwazi ambao ni rahisi kwa wakimbizi kuingia hasa majira ya usiku.
Eneo hilo lina msururu mrefu na njia kuu kutoka Asia ya kati kwenda Ulaya ambalo limekuwa na udhibiti ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Lakini nchi za Ulaya, pamoja na Uturuki zinahofia kurejea kwa ghafla kwa wanamgambo wa Taliban na kuchukua utawala kunaweza kubadili hali ilivyo sasa.
Bara Ulaya lilikabiliwa na mzozo wa wakimbizi wa mwaka 2015 uliosababishwa na vita vya Syria, na viongozi wa Ulaya sasa wanataka kuepuka hali hiyo ya wakimbizi na wahamiaji kuingia kwa wingi isitokee tena.
Isipokuwa kwa wale waliosaidia majeshi ya magharibi katika vita vilivyodumu kwa miongo miwili nchini Afghanistan, raia wengine wanashauriwa kama ni lazima kuondoka basi wahamie nchi za Jirani.