Uchunguzi huo unaangalia uhusiano wa chanjo ya Moderna dhidi ya COVID-19 na uwezekano wa kuhusishwa na hatari kubwa za maradhi ya moyo kwa vijana, kuliko vile ilivyodhaniwa awali.
Gazeti hilo lilinukuu vyanzo ambavyo haviruhusiwi kuzungumza kuhusu uchunguzi unaofanywa na idara ya uangalizi wa ubora wa chakula na dawa Marekani (FDA) na kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa Marekani (CDC).
Marekani inatumia takwimu kutoka Canada, gazeti hilo lilisema, ambapo inapendekeza kuwa vijana haswa wanaume chini ya umri wa miaka 30 au zaidi, ambao walichanjwa chanjo ya Moderna wanakabiliwa na hatari kubwa ya magonjwa ya Moyo, kuliko wale ambao waliopata chanjo ya Pfizer.
Akaunti ya Post pia ilisema maafisa wa FDA na CDC, pia wanachunguza takwimu kutoka Marekani kujaribu juu ya ongezeko la hatari, kwa watu wa Marekani.