Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:10

Ukraine: Wanawake, watoto na wazee waondolewa katika kiwanda cha Azovstal

Maria akilia baada ya kukutana na rafiki yake katika kituo cha wakimbizi cha Zaporizhzhia. Alikuwa katika maficho ya njia za chini ya ardhi za kiwanda cha chuma cha Azovstal kwa miezi miwili huko Mariupol hadi walipookolewa katika operesheni inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa.

Wote wanawake, watoto na wazee wameondolewa kutoka katika kiwanda cha chuma cha Mariupol  kilichozingirwa na majeshi ya Russia, kulingana na mwandishi wa VOA mjini  Kyiv, Anna Chernikova.

Wote wanawake, watoto na wazee wameondolewa kutoka katika kiwanda cha chuma cha Mariupol kilichozingirwa na majeshi ya Russia, kulingana na mwandishi wa VOA mjini Kyiv, Anna Chernikova.

Kiwanda cha chuma cha Azovstal cha enzi ya Umoja wa Sovieti, kilikuwa ngome ya mwisho ya majeshi ya Ukraine katika mji wa Mariupol, ambacho kilikuwa ni alama ya upinzani dhidi ya juhudi pana za Russia ya kuteka maeneo ya mashariki na kusini mwa Ukraine katika vita vinayoendelea kwa wiki ya 10, Reuters imeripoti.

Mtoto wa kiume aliyekuwa katika maficho ya kiwanda cha chuma cha Azovstal kwa wiki kadhaa akisubiri katika basi kupelekwa katika hoteli baada ya kusafiri kwa siku mbili kwenye msafara wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kutoka Mariupol hadi Zaporizhzhia, May 3, 2022. (Yan Boechat/VOA)

Iryna Vereshchuk, naibu Waziri Mkuu wa Ukraine, ameandika katika ujumbe wa mtandao wa telegram “sehemu hii ya operesheni ya kibinadamu ya Mariupol imekamilika.”

Umoja wa Mataifa, ambayo inaongoza juhudi za uokoaji ikishirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, haijathibitisha kama operesheni hiyo imekamilika.

“Umoja wa Mataifa wako katika eneo hilo, wakiwa na wenzetu kutoka ICRC, wakishughulikia kuweka njia salama zilizokubaliwa na pande zote katika mzozo huo.

Hii inajumuisha Azovstal na maeneo mengine yanayoizunguka Mariupol. Umoja wa Mataifa utatoa maelezo zaidi ya operesheni hiyo wakati itakapo kamilika,” alisema Saviano Abreu, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayo Ratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).

Reuters imeripoti kuwa mashambulizi mazito ya mabomu yakiendelea, wapiganaji na raia walikuwa wamekwama kwa wiki kadhaa katika maficho ya chini ya ardhi na njia zinazopita chini ya ardhi katika eneo la kiwanda hicho, wakiwa na chakula, maji na dawa kidogo.

Majeshi ya Russia yakisaidiwa na vifaru na makombora walijaribu tena Jumamosi kuingia Azovstal, kikosi cha jeshi la Ukraine kimesema, ikiwa ni sehemu ya shambulizi la kinyama kuwaondoa watetezi wa mwisho wa Ukraine kutoka katika mji wa kimkakati wa bandari katika Bahari ya Azov.

Mariupol umebakizwa kuwa magofu kutokana na wiki kadhaa za mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Russia, na kiwanda cha chuma kwa kiasi kikubwa kimeharibiwa. Makundi kadhaa ya raia yameondoka kutoka katika eneo la kiwanda wiki iliyopita wakati mapigano yalipositishwa.

Shirika la Afya Duniani(WHO) linakusanya ushahidi wa uchunguzi wa uwezekano wa uhalifu wa kivita kutokana na mashambulizi ambayo inasema imerkodi yaliyofanywa na Russia katika vituo vya afya huko Ukraine, ilieleza huko Kyiv Jumamosi.

XS
SM
MD
LG