Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 08:07

Watu 50 wamehamishwa kutoka eneo lililozingirwa la Azovstal, Vikosi vinavyounga Russia mkono vyasema


Watu waliohamishwa kutoka kiwanda cha chuma mjini Azovstal, Ukraine.
Watu waliohamishwa kutoka kiwanda cha chuma mjini Azovstal, Ukraine.

Vikosi vinavyoiunga mkono Russia vimesema zaidi ya watu 50 wamehamishwa leo kutoka eneo lililokuwa linazingirwa la kiwanda cha chuma cha Azovstal kwenye mji wa Mariupol ambako idadi kubwa ya raia wamekwama kwa wiki kadhaa katika mapigano ya Ukraine .

Makao makuu ya ulinzi wa eneo la jamhuri ya watu wa Donetsk iliyojitangazia yenyewe ilisema kwa njia ya telegram kwamba jumla ya raia 176 sasa wamehamishwa kutoka kwenye kiwanda hicho cha chuma.

Hata hivyo shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha habari hiyo mara moja.

Takriban watu 50 wamehamishwa siku ya ijumaa kutoka kwenye kiwanda cha chuma kilicholipuliwa karibu na bezimenne katika eneo lililojitenga DPR ambalo vikosi vyake vinapigana na wanajeshi wa Russia kwa ajili ya kupanua udhibiti wao katika maeneo makubwa ya mashariki mwa Ukraine, kwa mujibu wa vikosi hivyo.

Darzani za raia pia walihamishwa mwishoni mwa wiki jana.

Mariupol imekabiliwa na mashambilizi makali katika wiki kumi za vita. Kiwanda hicho ndio cha mwisho kubaki katika mikono ya wapiganaji wa Ukraine.

Mamia ya watu walikwama huko kwa wiki kadhaa wakiwa na chakula na maji au dawa kidogo.

Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky alisema katika ujumbe wake wa video ijumaa usiku kwamba Ukraine ilikuwa inafanya kazi katika juhudi za kidilpomasia kuokoa watetezi katika kiwacha cha chuma.

Haijaweka bayana ni wapiganaji wangapi wa Ukraine waliobaki huko.

XS
SM
MD
LG