Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 07:42

EU yatangaza vikwazo vipya ikiwemo kupiga marufuku mafuta ya Russia


Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen

Umoja wa Ulaya (EU) umependekeza hatua kali zichukuliwe dhidi ya Russia ikiwemo kupiga marufuku kabisa kununua mafuta yake na vikwazo kwa washukiwa wa uhalifu wa vita.

Rais wa tume ya EU Ursula von der Leyen amesema mpango huo una lengo la kuweka shinikizo kali kwa Russia wakati ikipunguza uharibifu Ulaya.

Mafuta ghafi ya Russia yataondolewa ndani ya miezi sita.

Rais wa tume ya Umoja wa EU anaeleza kuwa:“ tutahakikisha kwamba tunaondoa mafuta ya Russia kwa utaratibu, ambao utatuwezesha sisi na washirika wetu kuwa na njia nyingine za kupata ugavi wa mafuta na wakati huo huo kuwa makini kuhakikisha kwamba tunaondoa matokeo mabaya kwenye soko la dunia.

Ndiyo maana tutaondoa usambazaji wa Russia wa mafuta yasiyo ghafi ndani ya miezi sita na bidhaa ghafi ndani ya mwaka mmoja. Hii itaweka shinikizo kwa Russia na wakati huohuo, hili ni muhimu, tunaondoa uharibifu kwetu na kwa washirika wetu kote ulimwenguni kwa sababu ili kuisaidia Ukraine lazima tuhakikishe kwamba uchumi unabaki kuwa imara.”

Maafisa wa kijeshi waliohusika katika tuhuma za uhalifu wa vita, huko Bucha na Mariupol pia watakabiliwa na vikwazo vipya.

Rais Leyen amesema: “ leo tunawakilisha kwa mara ya sita vikwazo dhidi ya Russia. Kwanza, tunaorodhesha maafisa wa juu na watu binafsi waliofanya uhalifu wa vita huko Bucha na wale wanaohusika na kuwazingira binadamu katika mji wa Mariupol. Hii inatuma ishara nyingine muhimu kwa wahusika wote wa Kremlin. Tunajua wewe ni nani. Tutawawajibisha. Hautalikimbia hili.”

EU kwa wiki kadhaa umekuwa ukilenga ni jinsi gani itajiondoa kwenye mafuta na gesi ya Russia.

XS
SM
MD
LG