Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:03

Tanzania : CHADEMA yatangaza kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa


Chama cha kikuu cha Upinzani nchini Tanzania cha CHADEMA kimetangaza rasmi Alhamisi kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakayofanyika November 24.

Chama hicho kinadai kuwa wakishiriki watakuwa wanahalalisha ubatili uliojitokeza katika zoezi zima la uchaguzi kuanzia uandikishaji, wapiga kura hadi wagombea kuwasilisha maombi ya kutaka kuwania nafasi za uongozi.

Awali vyama vya upinzani nchini humo vililalamikia mchakato wa wagombea wa nafasi mbali mbali wakiwashutumu wasimamizi wa uchaguzi huo kuhusika na njama za kuwaengua wateule wa vyama hivyo vya upinzani.

Vyama vya CHADEMA na Act Wazalendo ni miongoni mwa vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa vikitoa malalamiko hayo kwa sehemu kubwa vikidai kuhujumiwa na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika shughuli ya kuwapitisha wagombea wao.

Tumaini Makene ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA anasema kamati kuu ya chama chao ilikutana kujadili mustakabali wa uchaguzi huu na na hivyo kufanya maamuzi ya kuwa hakuna haja ya kushiriki katika zoezi ambalo lina dosari nyingi sana kiasi kwamba uchaguzi mzima hautakuwa huru na wa haki.

Act Wazelendo kinaeleza kuwa wagombea wao takriban elfu mbili wameenguliwa kugombea katika uchaguzi huo bila sababu za msingi

XS
SM
MD
LG