Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu Dar es Salaam, Tanzania Charles Kichere ataapishwa siku ya Jumatatu kushika nafasi hiyo.
Taarifa ya ikulu imesema Profesa Mussa Assad kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano kinaishia kesho.
Kichere ambaye alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli. Rais baadae alimteua tena kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Juni 8, 2019.
Akisoma taarifa ya uteuzi huo Jumapili, Balozi John Kijazi amesema nafasi ya Kichere itajazwa na Katarina Revocati ambaye alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.
Pia, Rais Magufuli amewateua Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Kanali Francis Mbindi kuwa kamishna wa kazi ofisi ya Waziri Mkuu na majaji 12 wa Mahakama Kuu.
Sherehe fupi za kuapishwa wateule wote hao zitafanyika ikulu Jumatatu asubuhi, majira ya Afrika Mashariki.