Ripoti hiyo iliyowasilishwa Jumatano bungeni mjini Dodoma, pia imebainisha matumizi mabaya ya fedha kwa vyama vya siasa na kudai kuwa katika ripoti iliyopita ni mapendekezo 80 pekee kati ya 350 yaliyofanyiwa kazi kikamilifu.
Prof Assad alieleza: "Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma."
CAG amesisitiza kuwa neno 'dhaifu' ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. na litaendelea kutumika.
Mahojiano maalum na CAG
Miaka iliyopita, CAG alikuwa anatoa mukhtasari huo kwa waandishi wa habari bungeni mara tu baada ya ripoti yake kuwasilishwa kwenye chombo hicho.
Wakati anazungumza na waandishi Profesa Assad aliwaambia kuwa "nimetazama kwenye TV ripoti imewasilishwa bungeni na 'order paper' (karatasi yenye orodha ya shughuli za kikao cha Bunge) ninayo hapa inaonyesha ripoti imekabidhiwa bungeni Jumatano, asubuhi, na nimetazama ikiwasilishwa.
Pia amesema mwaka 2019 ofisi yake imetoa ripoti yake kwa CD ili kuepuka gharama nyingi za uchapishaji.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.